Книга - Robo Mwezi

a
A

Robo Mwezi
Massimo Longo E Maria Grazia Gullo


ROBO MWEZI: Dunia ambayo Elio anatorokea huenda isiwe kipande cha mawazo yake, lakini utando uliofumwa kwake. Wakati wa likizo kijijini atapata fursa ya kukutana na mlinzi atakayemfichulia ukweli. Kando na kundi la kuchekesha, wa ukweli na wa kimawazo, atapambana ili kujipatia tena uhuru wake. Vituko vya mtoto huyo vitakufanya ufahamiane na mapepo, mlinzi, kifuli, vidonda, tulivu za miujiza, na utasafiri kote duniani ukitumia taa za trafiki,ukizunguka mbuyu au kupaa ndani ya mpira wa barafu







Robo Mwezi

Watumishi wa Campoverde



Imetafsiriwa na Kennedy Langat



Hakimiliki © 2019 M.G. Gullo – M. Longo

Picha ya jalada na michoro iliundwa na kuahiririwa na Massimo Longo

Haki zote zimehifadhiwa

ISBN

ISBN-13:


JEDWALI YA YALIYOMO





Dibaji



"Kila kitu kitakuwa sawa, wewe ni mvulana mkubwa sasa....Rudi na ucheze na Watoto wengine. Tutakutana tena, ninakuahidi''

Mtoto alimtazama akitiririkwa na machozi alipoondoka mtu ambaye amekuwa akicheza naye tangu mwanzoni.

Mtoto alikimbia kurejea kwenye vijigari kwenye bustani iliyojuani, ambako alikwenda kucheza na watoto wengine jirani, huku fikra za rafiki ya kimawazo zikififia polepole.

Baada ya kujipenyeza kwenye mahali watoto wengine walikuwa, hatimaye angeweza kupanda kwa kitelezo. Hakupoteza hata muda na alianza kuteleza kwenda chini ya kitelezo, akisukuma kwa bidii kadri awezavyo. Hakuteleza hata hadi mwisho, wakati alipoona msichana mwenye nywele nyeupe akikimbia kutoka kwa mama yake na kuelekea kwenye miguu yake. Hakuweza kupunguza mwendo na alimgonga kwa nguvu.

Msichana huyo mdogo alipoteza mwelekeo na kugonga kichwa chake kwenye ukingo wa kitelezo.

Alijaribu kumfikia mtoto huyo msichana ili kuhakikisha kuwa alikuwa sawa, lakini akasukumwa kando bila huruma na mamaye, ambaye alikuja kumwokoa. Ghafula, kundi la babu na akina mama walikusanyika karibu na msichana huyo maskini.

Alipokuwa akijaribu kutambaa mbali na miguu ya watu wazima, alihisi kwamba alikuwa amezimia. “Mtu mmoja aliita ambulensi!” Huku sauti hiyo ikijitokeza kwa nguvu kwenye maskio yake, alianza kuingiwa na hofu. Alikimbia kuelekea msituni nyuma ya bustani.

Ghafula, kila kitu karibu naye kikawa giza. Upepo baridi ulikuwa umesheheni sauti za kutisha. Mistari asiyoijua ilianza kuchanganyika na mazungumzo ya wazazi kwenye bustani. Zilikuwa zikitoka nyuma ya kundi la miti, ambayo vivuli vyao virefu vilikuwa vinajidhihirisha. Kisha, sauti hiyo ambayo ilikuwa ikijitokeza kutoka pande tofauti ilizidi kuendelea kusikika. Alikuwa akimfikia zaidi na zaidi, hadi alipohisi kuwa ilikuwa ikinong'oneza maskioni mwake:



"Damnabilis ies iom, mirdo cavus mirdo, cessa verunt ies iom, mirdo oblivio ement, mors damnabils ies iom, ospes araneus ies iom…"

Aliweka kichwa chake kwenye mikono yake ili kutuliza sauti hiyo, lakini haikusaidia. Alipiga magoti na akafunga macho yake...



"Damnabilis ies iom, mirdo cavus mirdo, cessa verunt ies iom, mirdo oblivio ement, mors damnabils ies iom, ospes araneus ies iom…"


Sura ya kwanza



Anaepuka nikijaribu kumkumbatia……….



"Elio, Elio, njoo hapa! Nisaidie kuanua mboga kabla ya dharuba kuja, tafadhali."

Elio alikuwa amesimama wima akiwa amevalia viatu vyake vipya na alikuwa akimtazama mamaye, ambaye alikuwa akihangaika katika shughuli zake.

"Elio! Usisimame tu hapo! Chukua hii!" Alimtikisa na kuweka begi iliyojaa mboga kwenye mikono yake. Elio hakuwa na nia ya kufanya kitu kingine. Alipanda ngazi zilizoko nje ya jengo, akageuka na kufungua mlango. Alianza kutazama taa nyekundu ya lifti ambayo mwangaza wake haivumiliki. Kisha, akaacha kusubiri na kupanda ngazi kwenda kwenye nyumba yake gorofani. Aliweka mboga kwenye meza ya jikoni na kwenda moja kwa moja hadi chumba chake cha kulala kusikiza muziki kitandani.

Mara tu alipopanda gorofani mamake akaenda kumtafuta. Alisimama mlangoni akipiga kelele: “Unafanya nini? Hatujamaliza bado, njoo unisaidie!".

"Sawa, nko njiani..." akajibu Elio bila kusonga. Kwa kweli alitaka tu kumwepuka. Giulia akatoka, akitarajia kwamba mara hii itakuwa tofauti. Hakuwa na matumaini. Alikuwa akihangaika kumtia moyo mwanawe, ambaye alikuwa akizidi kuwa mwenye kutojali. Kutoka Mlangoni, aliweza kusikia wazi hatua za dadaye huku akimwita kwa sauti ya furaha. "Elio! Elio! Ondoa makalio kitandani na uje usaidie mama. Anakusubiri huko chini." Alimfokea huku akifahamu kwamba itakuwa bure tu. Elio hakusonga hata inchi moja. Badala yake, aliongeza sauti ya muziki na kuendelea kutazama dari, kana kwamba hakuna kinachotendeka. Giulia, ambaye alikuwa amechoka kutokana na mabishano na mwanawe kuliko kutokana na uchovu, mwishowe alilazimika kupandisha mboga akisaidiana na bintiye, Gaia. Huku akipanda ngazi ya jengo hilo lililo na orofa tano, ambako lifti yaonekana kutofanya kazi kila siku (na kwa kejeli, siku sote haifanyi kazi wakati anapotaka kubeba mboga kupanda ngazi kwenda juu), aliendelea kufikiria kuhusu Elio. Jengo hilo lilipakwa rangi nyeupe na ya machungwa, kama majengo mengine ya baraza la Gialingua, mtaa ambao walikuwa wanaishi. Familia ishirini ziliishi katika mtaa huo, na zilikuwa zimegawanywa katika gorofa ishirini zilizoangalia pande tofauti ya jengo lenyewe.

"Hii ni mara ya mwisho unafanya hivi!" akamfokea akiwa jikoni. "Tutatatua hii punde to baba yako atakaporejea nyumbani!"

Elio hakuwa hata anamsikiliza kwa kuwa alikuwa amezama katika muziki huo wa kuchukiza. Hakuna na hakuna anayeweza kutikisa hisia za uchoshi na ubishi aliousheheni. Dunia yake isiyopendeza ilikuwa kama makazi kwake. Huo ndio ulikuwa utu wake na dunia ililazimika kumzoea. Gaia alikuwa tofauti kabisa: alikuwa na umri wa miaka kumi na mitano, ana macho angavu na nywele fupi nyeusi. Saa ishirini na nne hazikotosha kwake kushughulikia maslahi yake yote.

Giulia alikuwa mwanamke mwenye nguvu pia. Lakini, kinyume cha bintiye, alikuwa na nywele nyeupe zilizopindika, alikuwa mnene kiasi lakini mwepesi na aliyejitolea. Alikuwa mama wa kawaida mwenye umri wa miaka 42: kila wakati alikuwa na ratiba ngumu akijaribu kudumisha usawa kati ya kazi na familia.

Ilikuwa chakula cha jioni. Hata hivyo, hakuna kelele zilizosikika kutoka chumba cha kulala cha Elio. Kwa kweli, hajasonga tangu alipokimbia kujitosa kitandani na kuvaa vipokea sauti vinavyobanwa kichwani.

Alisikia sauti ya ufunguo katika kufuli wa mlango wa mbele. Wakati uo huo, huku mlango ukiwa bado haujafungwa vizuri, sauti ya hamaki ya Giulia tayari ilikuwa imemkera mumewe:

"Hatuwezi kuendelea kufanya hivi!"

"Mpenzi, wacha niingie chumbani kwanza..."

Giulia alimbusu mumewe na kurudi kulalamika.

"Ni kumhusu Elio, sivyo?" alisikika kama aliyekata tamaa wakati alipouliza.

"Ndio, ni yeye." akajibu Giulia.

Wakati uo huo, Carlo akatoa mkebe wa chakula ndani ya begi lake ambalo alikuwa akienda kuacha jikoni. Kisha, alikuwa akienda kuweka mkoba wake kwenye kabati la nguo. Ndani ya mkoba huo, kila wakati angeweka jezi ya ziada kwa kwa sababu ya mawimbi ya joto ambayo yalikuwa yakipiga eneo hilo mwezi huo wa Mei.

Alikuwa mwema, mwenye umri wa miaka arobaini na mbili, mrefu na mwembamba. Nywele zake zilikuwa zimegeuka kijivu, lakini wakati mmoja zilikuwa zinafanana na za bintiye. Uso wake uliochongoka ulikuwa wazi: kwenye pua lake lililofanana na mdomo wa ndege alikuwa akivalia miwani duara ya chuma.

"Tuizungumzie kumhusu baadaye?" kwa upole alimmwuliza bibiye, akitarajia kwamba atasononeka.

"Ndio, uko sahihi mpenzi." alijubu, lakini aliendelea kulalamika hadi wakati chakula cha jioni kilipoandaliwa.

Kwa bahati, Gaia hakuacha kuongea kuhusu siku yake, akichukulia machungu yake madogo kwa njia ya kutia moyo.

Giulia alikuwa amemaliza kuandaa mezani wakati aliposema:

"Umwite Elio."

" Haina maana na unaifahamu." alijibu. "Unajua hatasonga hata inchi moja, isipokuwa aitwe na baba..."

Giulia, kisha akamgeukia mumewe:

"Ameshinda katika chumba hicho tangu nilipomrudisha nyumbani kutoka shule. Anazidi kuwa mbaya."

"Si tulisema atakuwa akirudi nyumbani mwenyewe kuanzia sasa na kuendelea?"

"Nilikuwa katika eneo hilo...

Nilikuwa nikinunua mboga..."

"Kila siku unatoa vizingizio ili kumlinda, lakini tena unalalamika kuhusu tabia yake!"

Carlo alikuwa akitikisa kichwa chake kama ishara ya kutokubali. Kisha, akaamka kwenye kochi na kwenda kwenye chumba cha watoto.

Aliingia kwenye chumba hicho cha kulala bila kubisha hodi na kumpata Elio katika mahali papo hapo ambako Giulia alikuwa amemwacha. Alikuwa akitazama dari kwa macho yaliyofunikwa, na alikuwa bado amevalia vipokea sauti vya maskio vyeupe vya Wi-Fi, na hata alikuwa hajavua viatu vyake.

Carlo hakuamini kwamba alikuwa mvulana yule yule ambaye angeandamana naye kila wakati kwa safari ya kuendesha basikeli. Sasa alikuwa na umri wa miaka kumi na sita, alikuwa mrefu kama yeye, na macho yake ya kijani kibichi bado yalikuwa mazuri, lakini yalionekana yaliyokufa. Katika miaka michache iliyopita, amekuwa akiugua unyongovu. Carlo alikuwa hajasikia kicheko chake kwa muda mrefu, hivi kwamba alikuwa amesahau jinsi inavyosikika. Alikuwa akijuta kwamba hangeweza kukaa naye kwa muda mrefu kama awali. Hata hivyo, alikuwa na shaka kwamba, kufikia sasa, umakinifu wake utathaminiwa.

Kwa bahati mbaya, miaka kadhaa kabla ya hayo, Carlo alikuwa amepoteza kazi yake kufuatia shida za kifedha. Kufuatia kuongezeka kwa mapato, kampuni hiyo ilihamishwa ngambo, kama kampuni nyingine nyingi.

Carlo alijitahidi kupata kazi. Hatimaye, akapata kazi katika mji tofauti. Kila siku alilazimika kusafiri muda mrefu na kubadilisha njia ya usafiri mara kadhaa, na kusababisha kuwa mbali na familia yake kwa saa nyingi kila siku. Hurejea nyumbani akiwa amechoka na akili yake kusubaa. Baada ya chakula cha jioni, analala kwenye kochi na bila shaka kuzama kwenye usingizi licha ya jaribio ya kutaka kuwa macho.

Carlo alidokeza kuwa Elio anapaswa kutoa vipokea sauti vya maskioni. Elio alikubaliana naye tu ili kuepuka kukemewa.

"Ni wakati wa chakula cha jioni. Njoo ule." Aliamuru. "Mamake alisema kuwa umekaa hapa tangu saa kumi jioni!"

Elio aliamka kutoka kitandani, na huku akiangalia chini alitembea kupita mbele ya babaye. Na kisha akatembea kuelekea jikoni, bila hata kujaribu kujadiliana na babaye.

Gaia tayari alikuwa ameketi mezani ambayo alikuwa ameandaa na alikuwa akiwatumia ujumbe rafiki zake na kufanya mipango nao.

Elio aliketi mbele ya dadaye. Walakini hakuongea neno hata moja naye wakati wote wa chakula cha jioni.

Chakula cha jioni kilibainika kuwa kisicho cha furaha. Kila mtu alikuwa akiongea kuhusu matukio yao ya kila siku, isipokuwa Elio, ambaye alikula vipande vichache vya nyama na kurejea kwenye chumba chake haraka iwezekanavyo. Mamaye alisikitishwa na ishara hiyo, na babaye pia ambaye alionekana kukunja uso.

Wakati Giulia na Carlo waliachwa chumbani wakati walikuwa wanaondoa sahani mezani, walianza kuzungumzia mada iyo hiyo ya awali: tabia mbaya za mwanao.

"Ni nini tunafanya vibaya? Hata siwezi kuelewa! Gaia ni mtu tendaji, mwenye furaha na mwenye hiba!" alisema Giulia

"Nilimpuuza sana!" Carlo alijilaumu kama kawaida.

"Wewe si baba pekee duniani ambaye analazimika kuwa mbali na nyumbani kwa saa nyingi. Mimi, kwa upande mwingine, niko nyumbani kila alasiri" Alirudia tena kwa kuwa hakutaka mumewe kuhisi kuwa na mzigo begani.

"Sio swala la tabia, Giulia, kwa sababu Elio hakuwa hivi awali, na unaijua!"

"Natamani pia kwamba asingekuwa hivi, Carlo, lakini watoto hubadilika wanapokua. Na kisha, wanazidi na kuzidi kuwa wabaya zaidi, sivyo? Akiwa shuleni ni balaa. Natarajia kuwa hatapinga, lasivyo hatutaweza kumpeleka kwenda kambi ya majira yajayo ya joto...hatutaweza kumruhusu kwenda shule wakati wa kiangazi...hatafurahia!"

"Giulia, watoto wengine kwa kawaida huburudika shuleni wakati wa kiangazi. Watoto wa Francesca na Giuseppe wanafurahia sana. Unafahamu vyema kuwa hatafanya chochote kwenye kambi ya majira ya joto! Tunahitaji kutafuta chaguo jingine, kitu ambacho kitamfanya apambane. Hata haonekani kuwa na furaha. Je! Unakumbuka jinsi tulivyokuwa na nguvu wakati tulipokuwa na umri sawa na yake?"

"Bila shaka, naikumbuka!" Mamangu angefoka kwenye mlango wetu kwamba chakula cha jioni kimekuwa tayari. Lakini, mara nyingi, hata singemsikia kwa kuwa nilikuwa na shughuli nyingi kwenye bustani nikijibingirisha kwenye nyasi. Tulikuwa na furaha na huru. Kwa kweli hatuwezi kumpa maisha kama hii mjini. Walakani, hajui jinsi ya kufurahia kambi ya majira ya kiangazi. Hana rafiki, hakuna tunayeweza kumwalika na kumsaidi kuponya tabia hii ambayo anaishi. Haruhusu mtu yeyote kushikamana naye. Wakati mwingine najiuliza jinsi anavyohisi kuhusu sisi. Anakwepa ninapojaribu kumkumbatia..."

"Giulia, vijana hawataki kukumbatiwa na mama zao. Nina uhakika bado anatupenda, lakini hatuwasiliani naye kwa njia mwafaka. Tunahitaji kutafuta njia mpya. Tunahitaji kutafuta njia ya kumuamsha. Labda, angezungumza na Ida? Ana wavulana wawili wadogo. Labda anaweza akatupatia ushauri mzuri. "

"Unaogopa anaweza geuka kuwa kama Libero? Kwamba anaugua ugonjwa unaorithiwa wa kisaikolojia?"

"Hapana, kwa Libero ilikuwa tofauti. Matatizo yake yalitokana na kifo cha babaye. Lakini matukio hayo yanafanana na jinsi Ida anavyofahamu huenda ukafaa. Alifanya miujiza na kijana huyo baada ya kuhamia kijijini. Na alifanya yote hayo pekee yake! na shamba ilisaidia pia."

"Ndio, umjulishe hayo. Naamini dadako. Ana njia yake ya kuangalia mambo, na ninapenda."

"Tutaipata ripoti ya shule lini?" Carlo akamwuliza bibiye.

"Juni 19..."

"Tutakuwa tumechelewa kuamua kitu cha kufanya. Unapaswa kuuliza mwalimu wake wa Italia kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na wewe. Lazima tuamue ni wapi tunapeleka watoto wetu. Maombi ya kujiunga na kambi ya majira ya kiangazi na shule ya majira ya kiangazi yatafungwa kabla ya tarehe 19." alipendekeza Carlo.

"Ndio, umesema ukweli. Tunahitaji kuwa na uhakika wa hali hiyo, ingawa hafanyi vibaya shuleni. Ni vile tu haweki royo yake katika chochote anachokifanya. Unafahamu kwamba wapangaji wapya wameingia orofa ya pili? Waonekana kuwa watu wazuri. Bi Giovanna aliniambia walihamia hapa kutoka Potenza. Hiyo ni mbali! Hakika haitakuwa raisi kwao mwanzoni. Wana mwana aliye na umri sawa na Elio. Nitamwalika aje mchana fulani..."

Giulia kisha akagundua kuwa Carlo, ambaye alikuwa amelala kwenye kochi, tayari alikuwa amezama usingizini.

"Njoo, mpenzi, twende tukalale kitandani." Alimnongoneza kwa upole ili amwamshe.


Sura ya pili



Mnong'ono wa baridi ulikuwa ukimsumbua



Elio alikuwa amesimama kwenye njia pana ya miguu mbele ya shule yake. Watoto wengine wote waliokuwa karibu naye walikuwa wakiongeza kasi, wanaposhuka katika gari za wazazi wao au wakifukuzana wakiwa njiani kwenda nyumbani. Yeye kwa upande mwingine alikuwa akiangalia kila mahali kwa wasiwasi kwa gari ya mama yake kana kwamba ndio njia yake ya kuishi, akitarajia kwamba hajaondoka baada ya kukutana binafsi na mwalimu wake wa Italia.

Baada ya kila mtu kuondoka katika yadi ya shule kwa muda mfupi, Elio aliacha kusubiri na kuanza kutembea kwenda nyumbani. Alichukia kutembea. Na alichukia hata zaidi kutembea chini barabara hiyo isiyovumilika iliyo na mstari wa miti ya ndimu inayounganisha shule na nyumba yao.

Alisubiri dakika chache zaidi na kisha akaamua kuelekea nyumbani pekee yake. Kisha, akamuru mguu wake kusonga mbele. Kwa mtu mwengine yule inaweza kuonekana kama kazi raisi, lakini kwa Elio, ambaye mawasiliano yake na miguu yake ilikuwa haba, ilikuwa mapambano.

Akageuka kushoto kupitia del Corso; akiwa kwa kona alijipata mbele ya barabara iliyonyooka ambayo aliidharau. Kijisitu cha miti ya ndimu ilipandwa kando kando ya barabara hiyo kuu. Kwa mtu mwengine yule ilikuwa tu kijisitu kizuri cha miti ya ndimu iliyochanua ambayo manukato yake yalibebwa na upepo, na kulifanya eneo hilo kunukia viruzi. Alipoanza kwenda chini kufuata mistari ya miti kwa ugumu, alihisi kuwa anafuatwa.

Aligeuka kwa haraka na kufikiria kuwa alikuwa ameona mnyama mweusi amejificha nyuma ya mti.

"Haiwezi kuwa" aliendelea kujirudia mwenyewe. "Je! Nimeona miwani katika pua la mbwa huyo wa ajabu?"

Kwa hofu akaendelea kutembea, huku akiona vivuli nyuma ya miti. Isitoshe, upepo ulikuwa ukivuma kupitia matawi. Mnongono wa upepo ulikuwa unamhangaisha; ilikuwa ikikuna maskio yake na kisha kukwama kwenye akili yake.

Hakuweza kuelewa maana ya sauti hizo. Huku akiwa ameshikwa na hisia hiyo mbaya, aliamuru mwili wake kujaribu na kukimbia. Alikuwa akitokwa na jasho, na akikimbia zaidi, sauti hizo zilizidi kuonekana kama zinamkimbiza na vivuli vikaonekana kuzidi kumkaribia.

Alianza kukimbia kwa kasi na kwa uwezo wake wote. Kisha, alisikia sauti ya kikatili ikimwamuru kuacha kukimbia. Aligeuka mara moja na kwa mara nyingine aliona kitu ya sura nyeusi ikijificha nyuma ya mti uliokaribu. Alikuwa tayari amefika makutano na barabara kuu, ambayo ingeashiria mwisho wa ndoto hiyo.

Hata hivyo, alihisi upepo baridi nyuma ya shingo yake. Aligeuka tena, mara hii bila kukimbia, lakini kitu kilimgonga vikali na kumtupa chini.

Elio alishtuka na kujikunja kama mpira huku kichwa chake kikiwa kwenye mikononi mwake.

Wakati uo huo, alisikia sauti anayoijua ikimwita:

"Elio! Elio! Je! Unafanya nini?"

Ilikuwa dada yake ambaye alikuwa akimkaripia. Alikuwa amekasirika kwa kuwa alikuwa amemkimbilia. Baadaye alitambua kuwa Elio alikuwa katika hali mbaya.

Alitulia na kuuliza:

"Unajisikiaje?"

Elio, baada ya kusikia sauti yake, akainua kichwa chake.

Gaia aligunduwa kuwa alikuwa amechanganyikiwa, anatoa jasho na uso wake ulikwajuka kuliko kawaida. Kwa sekunde, alijaribu kufikiria ni kwanini alikuwa akikimbia. Haikuwa kawaida kwake. Ilionekana kwake kwamba alikuwa akitoroka kitu au mtu. Wakati uo huo, alimsaidia kuinuka.

"Kwanini ulikuwa ukikimbia hivyo?" alimwuliza. "Kuna kitu kilikutisha?"

Gaia hakukumbuka mara ya mwisho Elio alikimbia. Elio hakujibu. Kitu pekee alichokitaka ni kuondoka barabarani haraka iwezekanavyo. Alipiga kona barabarani bila kusema lolote.

Gaia akamfuata akiwa na wasi wasi.

"Elio!" alimwita tena.

"Hakuna kitu!" akajibu Elio kwa ujeuri. "Kwa kweli hakuna kitu!"

Tabia ya Elio ilimfanya Gaia kukasirika tena.

"Hakuna kitu, eeh? Ulinikimbia sawasawa. Na bado, unasema hakuna kitu!"

Elio alimwomba msamahaili kuepuka majadiliano zaidi, only to avoid further discussions, ambayo ingechosha mwili wake hata zaidi.

"Samahani." alisema.

Misamaha hiyo ya juu juu iliishia kumkasirisha Gaia hata zaidi. Hata hivyo, aliendelea kutembea nyuma ya kakaye, huku akiwa na wasiwasi kumhusu.



Kufikia Jumapili asubuhi, Carlo na Giulia hatimaye walikuwa wamefanya uamuzi. Wakati walipokuwa wanatengeneza kiamsha kinywa, walikuwa wakiongea kuhusu wazo hilo wakati wakisubiri watoto kuamka

"Alikuwa mkarimu kutoa wazo kama hilo. Nataraji, hao watato watakuwa na tabia njema." alisema Giulia akiwa na tabasamu kubwa usoni.

Ilikuwa uamuzi ngumu kufanya, lakini Carlo na yeye walikuwa wanahisi shauku ya ajabu kuihusu, kwa vile walikuwa wamekubaliana nayo.

"Gaia atafurahi." alisema Carlo. "Elio, kwa upande mwingine, atasalia kutojali kama kawaida."

"Sina uhakika...Gaia alifanya urafiki na watoto wengine katika kambi ya majira ya joto. Atakasirika. Na kuhusu Elio, atachukia hata hivyo." akasema Giulia.

"Siwezi kusubiri tena. Nitawaamsha." akapendekeza Carlo kwa uthabiti, na kutembea kwenda vyumba vyao akiwaita kwa majina yao.

Hakuniruhusu hata kusafisha uso wao.

"Mama yako na mimi tuliamua kile utakachofanya wakati wa majira ya joto. Shule itafungwa Ijumaa na Jumapili Asubuhi mtapelekwa kwa kituo cha reli!"

"Lakini kambi ya majira ya joto haitaanza kwa majuma mengine mawili yajayo!" Gaia alisema kwa wasi wasi na kumtazama mama yake. Kutoka mlango wa jikoni, alikuwa akitazama kile kilichokuwa kikiendelea kwenye ushoroba.

"Kwa kweli, hutaenda kwenye kambi ya majira ya joto mwaka huu" akajibu Giulia na kwa kufanya hivyo, alithibitisha hofu ya Gaia. "Tulifikiri tutakupa fursa ya kutumia wakati wako wa majira ya joto kwa mtindo wa zamani; jinsi tulivyofanya wakati tulipokuwa na umri kama yako. "

"Hiyo inatakikana kumaanisha nini?" akauliza Gaia, wakati Elio alikuwa kimya na mwenye sura mbaya.

"Utakuwa nje, kimbia hadi upungukiwe na pumzi, ogelea kwenye bwawa na utumie usiku wa majira ya joto kwenye maonesho mtaani" akajibu Carlo kwa bintiye.

Gaia aliweza kuona wazazi wake wakiangaliana na kucheka, na kwa haraka akafikiria walikuwa wakiwafanyia mzaha.

"Acha kutufanyia mzaha. Mnashida gani asubuhi hii?"

"Hiyo si mzaha. Shangazi Ida amejitolea kuwakaribisha wakati wa majira ya joto." Hatimaye Carlo akafichua kwa watoto wake, ambao walikuwa wakimwangalia bila kuamini.

"Hii ni ndoto mbaya. Ninarudi kulala!" akasema Gaia, ambaye alionekana kukasirika.

"Nilifikiria utafurahi " akasema babaye.

"Kufurahi? Tayari nilikuwa nimewasiliana na rafiki zangu! Nimesubiri wakati wote wa msimu wa baridi!"

"Gaia, utapata rafiki kwa shangazi pia." Mtie moyo Giulia.

"Lakini kwanini nitake kufanya hivo? Ninapenda kuwa na rafiki katika kambi ya majira ya joto. Ninaweza kukaa nje na kupiga mbizi ziwani. Sitaki kuwa mahali pengine."

"Ndio, hutaki. lakini Elio anataka. Anahitaji kubadilisha hewar." Akaongeza Carlo.

"Nilijua!" akaropoka. "Ni kwa sababu ya Elio! Na mbona asiende kwa shangazi Ida pekee yake?"

"Hatutaki aende pekee yake." akasisitiza Giulia.

"Mimi si yaya wake!"

"Lakini wewe ni dada yake mkubwa. Mbona husemi kitu, Elio?" akauliza Carlo.

Elio hakusema lolote. Akainua mabega yake, na kuathiri akili ya Gaia.

"Hivyo? Hakuna? Hakuna swala muhimu wkako. Haya! ambia mama na baba kwamba hutafanya chochote shambani pia."

Elio aliinama na kukubaliana naye.

"Acha, Gaia! Acha kufanya hivi! Tayari tumeshaamua. Binamu yako Libero atakuchukua kituoni" tamatisha mazungumzo Carlo.

Gaia akakimbia, akionekana kufa moyo na kukasirika.

"Atakuwa sawa." akasema Giulia, akijua starehe ya maisha ya bintiye.

Elio alirudi kwenye chumba chake bila kutambuliwa.

Carlo alishangaa. Hata hivyo, alikuwa na uhakika kwamba uamuzi wao ulikuwa bora katika kwa miaka mingi.



Ijumaa ilifika haraka. Carlo alimchukua mpwa wake kutoka kituoni na kufurahi alipofikiria kumkumbatia tena.

Libero alikuwa na furaha, mvumilivu na mvulana asiye wa kawaida. Alikuwa mrefu na mwembaba, lakini mifupa yake haikudhihirikamwilini. Uso wake ulikuwa umepigwa na jua, mikono yake ilikuwa kubwa na alikuwa akifanya kazi katika shamba la familia yake. Macho yake ya kijani yalionekana wazi kwenye ngozi yake, na nywele zake fupi za kahawia zilikuwa zimegawanyika kama mtu aliye na umri wa miaka 50. Alimkumbatia mjomba wake kwa nguzu na tangu wakati huo hakuacha kuongea.

Carlo alikuwa akimwangalia akishangaa. Alikumbuka vizuri wakati Libero alikuwa mgonjwa, asiyejali na mwenye kukasirika haraka. Ingawa Libero hakuwa mwerevu sana, lakini maisha raisi aliyokuwa akiishi yalimfurahisha. Na Carlo alikuwa akitaka Elio akubali chanya ya binamu yake. Wakati uo huo, Libero alikuwa akisukuma pua lake kwenye dirisha la gari na alikuwa anauliza swali kuhusu kila kitu aliona njiani.

Kila mtu nyumbani alikuwa akimsubiri.

Giulia alikuwa na wasiwasi wakati alipokuwa akifunga vitu vya mwisho. Wakati umefika na alikuwa akijiuliza iwapo mambo yatakuwa mazuri. Licha ya hayo, yeye alikuwa mama yao na hakuweza kujizuia ila kuwa na wasi wasi.

Gaia, kwa upande mwingine, alikuwa amekubaliana na wazo hilo. Alikuwa anamkimbiza mama yake ndani ya nyumba akiwa na maelfu ya maswali: aliweza kuona nini? Angefanya nini shambani?

Elio nay eye hawakuwa wameenda shambani tangu walipokuwa watoto wakati wazazi wa baba yao walikuwa hai. Hawakuwa na kumbukumbu yoyote ya mahali hapo, isipokuwa kumbukumbu: mashamba, au manukato ya miti iliyo nyuma ambayo iliwasadia kucheza mchezo wa kujificha na kutafuta.

Baada ya mumewe kuaga dunia, shangazi Ida alijitahidi kurudisha maisha yake. Basi, aliamua hamia kwa wazazi wake pamoja na watoto wake na kutelekeza shamba lake la zamani.

Mara tu aliposikia sauti za funguo zikifungua kufuli, Gaia alikimbia kuelekea kwa binamu yake, ambaye alimwinua na kumzungusha kama ilivyo kwenye jukwaa la kujiburudisha. Gaia alitabasamu kwa kuwa hakutarajia maonesho kama hayo ya mapenzi.

"Habari, Libero. Umekuaje?" alimwuliza kwa uchangamfu binamu yake ambaye alikuwa hajaonana naye kwa muda mrefu.

"Vizuri, mpenzi." akajibu Libero.

Wakati uo huo, Giulia alijiunga nao na Libero alimsalimia kama muungwana, akimpa busu ya haraka mara mbili kwmashavu yote mawili.

"Safari ilikuwa aje?" akauliza Giulia.

“Vizuri sana, "ngombe huyo wa chuma" ina kasi sana na ina raha wakati unataka kusafiri; na jiji limejaa vitu vya kupendeza kuona. Ninafuraji kuwa hapa!"

"Tafadhali keti. Lazima umechoka. Je! Ungependa aiskrimu?" akauliza Giulia.

"Ndio, asante, Shangazi." Nimepokea kwa furaha Libero. "Wapi Elio?"

"Elio yuko katika chumba chake. Atakuwa hapa baada ya dakika chache." rakajibu Carlo. Alikuwa amekasirika kwa sababu mwanawe hakujisumbua hata kuja kusalimia binamu yake, ambaye amesafiri mwendo mrefu ili kumchukua. Alipoanza kutembea kuelekea kwenye chumba cha Elio,

Libero alianza kuongea:"Usijali, mjomba Carlo. Nitaenda. Nataka kumshangaza. Niambie tu chumba chake ni kipi."

Mara tu Carlo alipomwonesha chmba cha Elio, Libero akamka kuelekea mlangoni. Kilio cha furaha cha Libero kilisikika kwenye ushoroba wakati alipokuwa akimsalimia binamu yake.

Hata Elio, licha ya utulivu wake hakuweza kuepuka kukumbatiwa na Libero.

Gaia alimtazama mamaye na kunong'ona:

"Sikukumbuka kwamba alikuwa anaweza kudanganywa hivyo!"

"Usiseme hivyo." Maramoja akamkaripia Giulia. "Ni mvulana mzuri. Na ni mwema sana pia."

"Ndio, lakini... Unauhakika atatuendesha salama hadi tufike shambani." Bila shaka aliuzila Gaia.

"Kweli, hiyo atafanya!" akamtuliza Carlo. "Usimdharau. Yeye na mama yake anaendeleza kazi ya shambani. Yeye ana nguvu na ni mwerevu."

Wakati wa chakula cha jioni ulifika na kuendelea kwa furaha. Kwa kweli, Libero alikuwa amemletea sherehe zote na uchangamfu wa vijijini, ambayo ilithaminiwa san ana kila mtu isipokuwa Elio.

"Nasubiri sana kukuonesha huku." Alimaliza Libero baada ya kueleza mambo ya shamba kwa binamu yake.

"Una uhakika kwamba hutaki kukaa kwa siku kadhaa kabla ya kuondoka tena?" akauliza Giulia.

"Siwezi kumwacha mama pekee yake wakati huu wa mwaka. Kuna mambo mengi ya kufanya."

"Uko sahihi, Libero. Kwa kweli wewe ni mvulana mzuri." akamsifu Carlo, akimpapasa kwa upole begani.

"Unajua, mjomba Carlo, nilikuwa najiuliza kitu. Kabla ya kuja huku mjini, nilifikiria unatakiwa kupiga honi tu wakati wa dharura...."

"Ndio, hiyo ni kweli." akajibu Carlo. "Kwanini?"

"Kwa sababu inaonekana kila mtu hutumia kana kwamba walikuwa wanacheza muziki kwenye sherehe! Hawaachi kupiga honi!"

Kila mtu aliangua kichezo, isipokuwa Elio, ambaye alijiuliza iwapo Libero alikuwa akitania au la ...


Sura ya tatu



Aligundua kuwa mvulana huyo alikuwa ametishika, na akaangua kicheko



Asubuhi ya siku iliyofuata Libero alimtoa Giulia kwenye kitanda chake baada ya kujikwa kwenye zulia la ushoroba. Kwa hivyo, Giulia na yeye walijikuta wakila kiamsha kinywa kabla ya kila mtu kuamka. Wakati harufu ya kahawa safi ilipokuwa iliovamia chumba cha kulala cha Carlo, pia alielekea jikoni na kuanza kuelezea kile kilichokuwa kimemekabili Elio siku za hivi karibuni.

"Usijali." aliwahakikishia Libero. "Uzoefu huu wa nje utamsaidia. Na mama tayari ana mkakati! "



Mara tu walipofika kituo cha gari moshi, Giulia hakuweza kuacha kutoa mapendekezo na kuhakikisha kuwa watoto watakuwa na tabia nzuri.

Gaia hakuweza kusubiri; alikuwa amesisimika na mdadisi. Kwa upande mwingine, ilikuwa wazi kwamba Elio alikuwa akiburuzwa tu kwenye hayo. Zaidi ya hayo, pia alikuwa amebeba mizigo mizito ya Gaia kwa sababu tu Libero alimfanya kufanya hivyo: "Wanawake hawapaswi kubeba uzito!" alisema, ambayo ilisababisha Elio atumbue macho. Hakuweza kumvumilia binamu yake tayari.

Libero alikuwa amevaa suruali ya khaki, t-shati na kofia ya kujikinga ya baseball ya manjano, ambayo ilionekana isiyofaa kabisa kwa binamu zake. Zaidi ya hayo, alikuwa amebeba mizigo iliyobaki kwa wepesi kiasi kwamba inaweza ilikuwa haina kitu ndani.

Treni iliondoka kwa wakati ufaao. Hakuna mtu mwengine aliyekuwa ndani ya gari walilokuwa wametengewa. Baada ya Libero kupanga mizigo yote kwenye juu ya gari, alipendekeza:

"Gaia, andamana nami. Hebu tuende kwenye mgahawa wa gari na tupate kiamsha kinywa zaidi. Itakuwa safari ndefu na utahitaji nguvu zako zote. Elio anaweza kuchunga mizigo. Hata hakuna mtu atakayeikaribia. Ikiwa mtu atagusa, bweka! " alisema Libero kwa binamu yake. "Na ukiacha kukasirika, tunaweza hata kukuletea chakula..."

Gaia na Libero walitoka nje ya gari, na kumpa Elio faraja kubwa kwa kuwa alitaka kuwa peke yake.

Alikuwa akiangalia mandhari ya nje kupitia dirisha lake. Walikuwa wamesafiri kupita eneo la viwanda la jiji na walikuwa wameanza kuzungukwa na mashamba na milima ambayo ilikuwa ikibadilishana tena na tena.

Ghafla, kwenye kidirisha cha dirisha akaona sura ya mzee amekaa kwenye kiti cha kando kiti chake.

Aliingia lini kwenye gari? Hakusikia milango ikifunguliwa.

Mzee huyo alikuwa amevaa nguo nyeusi na alikuwa amevaa miwani isiyo ya kawaida puani. Alikuwa akisoma kitabu cheusi cha ngozi ambacho kilionekana kama cha karne moja kilichopita, ambacho kurasa zake zilitengenezwa kwa karatasi ya tishu. Kichwani alikuwa na kofia yenye kuta pana iliyokuwa inaficha uso wake. Mandhari yote ilikuwa isiyo ya kutuliza.

Elio hakugeuka, lakini alikuwa akimwangalia kupitia akisi kwenye kidirisha cha dirisha. Alihisi kuogopa kuwa peke yake na mtu huyo. Wakati huo kwa hakika alitaka binamu yake mkubwa na mwenye nguvu awe karibu naye. Walakini, yeye wala Gaia hawakuwa wakionekana.

Wakati uuo huo, mzee huyo alikuwa bado anasoma kitabu chake. Kila baada ya muda, angeangalia saa ya zamani ambayo alikuwa akiiweka ndani ya mfuko ulio kwenye kifua cha koti lake la kiuno, alilokuwa amevaa kwa maridadi ndani ya suti yake ya zamani.

Hii ilimkera Elio zaidi, ambaye aliendelea kujiuliza huyo mtu anangojea nini au nani. Hakika lazima ilikuwa ni kitu cha umuhimu wa ajabu kutokana na jinsi alivyokuwa akiangalia saa yake kila wakati.

Ghafla, baada ya kuangalia saa tena, yule mzee alifunga kitabu chake na kuinama ili kutoa kitu ndani ya begi jeusi alilokuwa akiiweka katikati ya miguu yake. Alipokuwa akiinama chini, suruali yake ilipanda juu kidogo na kufunua vifundoni vyake vyeusi na soksi fulani nyembamba nyeusi ambazo zilionekana kama manyoya nyeusi.

Elio hakuweza kuzuia hofu yake na akaanza kutetemeka. Alipokuwa akiangalia ndani ya begi lake mwenyewe,mzee huyo akaangua kicheko kana kwamba alitambua hofu ya Elio. Kilikuwa kicheko kirefu, cha kina na cha huzuni ambacho kilisikika masikioni mwake. Elio aliziba masikio yake kwa mikono kujaribu kuzuia kusikia kelele hizo. Alifunga macho yake ili kuepuka kutazama akisi ya mtu huyo kwenye kidirisha cha dirisha na kuanza kusali: "Libero, rudi. Libero, rudi. "

Kisha, mlango wa gari unaotumia mtambo ulifunguliwa ghafla.

"Elio, unafanya nini? Je! Ulipata maambukizi ya sikio jijini? Usituambukize sisi wananchi na virusi hivyo vya mijini! "

Elio alishtuka. Halafu, baada ya kutambua sauti changamfu ya Libero, aligeuka nyuma na kumwona binamu yake akicheka; alikuwa ameshika begi lililokuwa na bidhaa alizonunua na kinywaji laini mikononi mwake. Gaia alikuwa amesimama nyuma yake na alikuwa akiuma kwa mkoromo kubwa.

Hakukuwa na dalili ya mzee huyo. Alipotea tu jinsi alivyokuwa ameonekana hapo awali. Kila kitu chake kilipotea: kitabu chake, saa yake na begi lake.

Libero aliketi karibu na Elio na baada ya kumpa mkoromo, aligundua alikuwa akitetemeka.

"Kuna kitu kilitokea?" Aliuliza.

"Nadhani ni ugonjwa wa mwendo tu." alidanganya Elio.

Gaia alielewa kuwa kaka yake alikuwa na shida moja na akaahidi mwenyewe atashughulikia shida hiyo kwa Libero.

Safari iliyokuwa imesalia ilikuwa ya utulivu. Libero alielezea tamasha la mavuno ambalo lingefanyiwa hivi karibuni na litahusisha vijiji vyote jirani. Litafanywa nje na jioni watachangamshwa na densi za kitamaduni kama taranta, na nyingine za kisasa.

Elio alikuwa akimwangalia dada yake na binamu yake, na akajiuliza ni vipi hawa wawili wameweza kuelewana haraka sana. Licha ya hayo, alifurahi kusafiri nao. Matukio yote hayo yalikuwa yakimpa wasiwasi. Alikuwa akiathiriwa na aina fulani ya njama dhidi ya hisia zake, au alikuwa akienda mwendawazimu?

Libero aliingiwa na woga kwani ilikuwa wakati wa kushuka kwenye gari moshi. Aliona kupitia kwenye dirisha nyumba ya Bibi Gina, ambayo ilichukuliwa kama sehemu ya kumbukumbu. Mara tu gari moshi liliposimama, akachukua mifuko. Halafu, baada ya Gaia kufungua mlango, kwa woga alitoka nje ya gari moshi kama wale ambao hawajazoea kusafiri mara nyingi.

Wenyeji wangechukulia sehemu hiyo kama kituo cha reli, lakini kwa kweli haikuwa chochote isipokuwa mahali tu pa kusimama katikati ya mahali pasipojulikana. Starehe pekee walizopewa na paa la jukwaa lililobomoka na mashine ya tikiti iliyovunjika ambayo ingeweza kupitisha ujumbe uliokwisha kurekodiwa ukisema "Uwe mwangalifu, kituo hiki hakiangaliwi. Jihadharini na wezi wa mfukoni ".

Libero akachukua pumzi nzito na kusema:

"Hatimaye, hewa safi. Karibu Campoverde. "

"Tayari ninahisi harufu ya mashamba." aligundua Gaia. "Unaweza, Elio?"

Elio hakuweza kuhisi tofauti yoyote ikilinganishwa na jiji, na alinyanyua mabega yake tu.

"Elio, chukua mzigo wa Gaia. Nitabeba hizo nyingine. "Akaamuru Libero.

Gaia bila kutarajia alifurahia tabia ya kiungwana ya Libero, ambayo kawaida ingemkasirisha. Lakini Libero alikuwa mkweli sana hivi kwamba alifurahishwa nayo na alikubaliana naye. Labda alikuwa na haraka ya kumchukulia kama mpumbavu...

Gaia na Libero walitembea mbele ya mashine ya tiketi ya kuzungumza, ambayo ilikuwa ikirudia rudia sentensi, na kisha wakaelekea upande wa chini wakitabasamu.

Ilibidi Elio anyakue mzigo mkubwa wa Gaia kwa mpini wake ili kushuka chini na kupanda ngazi za tombwe. Alikuwa amechoka kabisa.

Katika hatua chache za mwisho alifanya juhudi za mwisho akitumaini kwamba shangazi Ida angekuwa akingojea katika maegesho ya gari kuwapeleka nyumbani.

Lakini alipoingia kwenye maegesho, aligundua kuwa hakuna mtu aliyekuwa akiwasubiri. Libero, akiwa na Gaia kando yake, wakaelekea magharibi kwa kuambaa barabara nyembamba ambayo ilikuwa na lami duni. Mifereji miwili ilikuwa ikitiririka kando ya barabara na ilikuwa ikiitenganisha na mashamba ya mahindi upande mmoja na mashamba ya ngano upande mwingine.

Elio, ambaye alikuwa akihema, aliwapigia kelele kusimama kwa sekunde moja. Dada yake aligeuka akiwa amechanganyikiwa. Hangeweza kukumbuka mara ya mwisho kaka yake alizungumza kwa sauti kama hiyo, wala kupiga kelele namna hiyo.

"Gari la shangazi Ida liko wapi?" aliuliza Elio.

"Ah, samahani nimesahau kukuambia. Alinipigia simu akisema kwamba hawezi kuja. Camilla, ng'ombe wetu, yuko karibu kuzaa na mama hawezi kumwacha peke yake kwa sasa. "

"Camilla? Karibu kuzaa? Tutafanya nini? " Elio aliuliza akihema.

''Usiwe na wasiwasi. Ni maili nne tu na tutakuwa shambani. "Alijibu Libero kwa utulivu.

"Maili nne?" yalikuwa maneno ya mwisho ya Elio.

"Huamini! Mizigo ya dada yako ni ya kubeba! " alimtania Libero, kisha akarudi kutembea.



Kwa mbali nyumba kadhaa za kwanza zinaweza kuonekana.

"Ndio hapa! Nyumba ile nyuma ya mti wa cheri ni yetu. Ni shamba. "

Libero alionesha shamba jekundu la veneti lililo na mimea.

Bustani nzuri na iliyotunzwa vizuri iliyonyooka kutoka mlango wa mbele hadi laini za kuanikia nguo zilioaashiria mwanzo wa zizi. Zaidi ya hapo ni mashamba tu yake.

"Mama, tuko hapa!" alipiga kelele Libero, akiacha mizigo barabarani na kukimbia kuelekea zizi.

Shangazi Ida alitoka nje kupitia mlango wa mbele.

"Mpwa wangu wa kiume na wa kike!" alipiga kelele kwa furaha.

Gaia aliweka mikono yake shingoni mwake. Elio, ambaye alikuwa amechoka, alimsogelea na kumpiga busu shavuni. Nikuwe tu na heshima.

Ida alikuwa mtu mwenye umri zaidi ya miaka 50, lakini urembo wake wa asili ulikuwa haujafifia bado. Alikuwa mwanamke mwembamba, mwenye urefu wa wastani... Mwili wake ulikuwa uliwiana vizuri ingawa, mikono na miguu yake ilikuwa ya misuli na nguvu kuliko ya mwanariadha. Maisha magumu ya shamba ilikuwa mazoezi yake ya mwili ya kila siku. Alikuwa na nywele nyeupe zilizofungwa kama mkia wa farasi, na ngozi yake nzuri ingemfanya macho yake mazuri ya kijani kuonekana, kama ya mpwa wake.



Wakati huo huo, Libero alikuwa akirudi kutoka kwenye zizi, wote wakitabasamu.

"Camilla alizaa ndama wa kike! Maziwa zaidi kwetu! "

Shangazi Ida aliwaalika ndani ya nyumba. Meza iliandaliwa na harufu ya chakula kitamu cha mchana ilikuwa ikielea hewani. Watoto walikuwa na njaa na walikula vyakula vyote. Gaia hakuweza kuacha kumwambia shangazi yake hisia zake ambazo alikuwa amehisi wakati wote wa safari.

Baada ya chakula cha mchana, Gaia alimsaidia Ida kusafisha vyombo. Libero, kwa upande mwingine, alimburuta Elio kwenda shambani akimuuliza, au tuseme akiamuru amsaidie.

Wakati wa jioni, shangazi Ida alielezea kuwa chumba kilichoko darini kitakuwa chumba chao cha kulala cha majira ya joto. Walakini, kwa sasa walikuwa wakilala kwenye kitanda cha sofa sebuleni hadi chumba cha kulala darini kitapokuwa tayari.

Gaia alipanda juu ghorofani na kumfuata shangazi yake kuona chumba cha darini. Kwa upande mwingine, Elio alishtushwa na habari hizo mbaya za ziada.

Walikwenda juu hadi ghorofa ya kwanza, ambapo Ida na Libero watakuwa wakilala. Kwenye ghorofa iyo hiyo, pia kulikuwa na chumba cha kulala cha Ercole, binamu yake mdogo kabisa ambaye alikuwa amekwenda kwa kambi ya majira ya joto. Ida alionesha ngazi ya mbao iliyokuwa ikielekea kwenye dari. Hatapanda pale kwani tayari alikuwa amechoka kwenda juu na kurudi chini kwa ngazi. Kwa kweli, alikuwa tayari kwenye chumba hicho wakati wa mchana ili asafishe chumba hicho.



Wakati uo huo, shangazi Ida aliingia chumbani kwake na kwa siri alimwita Giulia, shemeji yake, ili amsasishe.

Simu haikulia hata mara mbili. Giulia alichukua mara moja.

"Habari mpenzi, unaendeleaje?" aliuliza Ida.

"Kila kitu kinaendelea vizuri, asante. Lakini niambie. Aliendaje? "

"Aliweza kutembea hadi hapa kutoka kituoni bila kuchoka. Alifikiri nitawapeleka nyumbani kwa gari. Libero alidanganya na kumwambia kwamba ng'ombe wetu, Camilla, alikuwa anakaribia kuzaa. "Akacheka Ida.

"Ningetaka kumuona akitokwa na jasho!"

"Baada ya kula chakula cha mchana ..." alianza kusema Ida, lakini Giulia akamkatisha.

"Je! Alikula chochote?"

"Ndio, alikula mara mbili."

Loo! Nyumbani hakuli hata mkate wa sandwichi. "

"Ni ngumu hata kama." Alisema Ida. "Lakini nina uhakika atakuwa sawa."

Kwenye usuli aliweza kusikia Carlo akiuliza maswali na kucheka.

"Michezo ya Runinga na video hakuna. Katika msimamo mkali wa mwisho. "



Elio, ambaye alikuwa amelala kitandani. Hakuweza kusogeza mwili wake. Ilikuwa imepita miaka kadhaa tangu atembee kiasi hicho.

Shuleni kila wakati alikuwa akitoa visingizio ili kuepuka darasa la mazoezi.

"Elio mwite dada yako hapa. Ninahitaji usaidi wa chakula cha jioni. "

Elio hakuamini kile alichokuwa amesikia. Hakuweza kuwa kwa kweli.

Lakini shangazi Ida aliongea kwa sauti ambayo haingeruhusu jibu lolote hasi.

"Elio, umesikia nilichosema?"

"Sawa." alijibu na kuendelea kuelekea ngazi ya ghorofa akiwa na uso zote mkali.

Alisimama chini ya ngazi ya mbao na kuanza kupiga kelele akiita jina lake.

Licha ya kelele za kaka yake, Gaia hakuwa akijibu.

Ndipo Elio, akiwa amekasirika zaidi, aliamua kupanda ngazi. Katika chumba cha dari kilichokuwa na giza alikuwa akihisi wasiwasi. Hatua kwa hatua, safari ya dari ilionekana kuwa haina mwisho. Punde tu alipofika na kichwa chake chini ya sehemu iliyoanguliwa, alianza kupiga kelele akiita jina la dada yake. Lakini tena, hakuna aliyejibu. Alijilazimisha kutembea hatua za mwisho. Na kisha kitu kutoka juu kilishika mkono wake.

Elio alikaa kimya, macho yake akiwa ameyafumba na sura ya kutishika usoni mwake.

"Unayo!" alipiga kelele Gaia, ambaye alikuwa amegundua kuwa Elio alikuwa na hofu.

"Ondoka kwangu. Umeniogopesha. Ungejibu. "

Gaia hakukubali hayo kwani alikuwa akivutiwa na kile alichokuwa amefahamu, na akasema:

"Dari hii imejaa vitu visivyo vya kawaida. Njoo hapa. Tazama hii..."

Elio alimaliza kupanda ngazi na kumfuata dada yake, ambaye alikuwa akivinjari picha za zamani.

"Hii ni ya kuchekesha." Alisema, akipitisha picha kwa Elio.

"Ni nini cha kuchekesha?" aliuliza Elio.

"Nini?" aliuliza Gaia. "Je! Humtambui?"

"Nani?!" aliuliza tena Elio.

"Ni baba!" alishangaa Gaia.

"Baba? Umesema kweli. Sikumtambui akiwa amevaa hivi. Anaonekana kama Libero. Wamevaa nguo zinazofana! "

Hatimaye, baada ya muda mrefu sana, alitabasamu. Wakati huo huo, Gaia, aliendelea kutazama picha nyingine.

"Umeiona hii? Nadhani ni Libero akiwa mchanga sana. Anaonekana kuwa sura nzito sana na mwenye huzuni hivi kwamba haionekani kama ni yeye. "

Picha hiyo ilionesha mtoto aliyeparara na dhaifu na mwenye amekaza macho.

"Anaonekana kutengwa sana" akasema Gaia.

Katika picha hiyo, alikuwa amesimama kwenye bustani na alikuwa ameshikilia mikononi mwake magari yake ya kuchezea. Picha hiyo ilikuwa imechukuliwa jioni na jua likiwa linatua nyuma yake. Libero alikuwa peke yake kwenye picha, hata hivyo kulikuwa na kivuli cha pili kando yake.

Elio aliiona na kwa wasiwasi akasema:

"Je! Unaweza kuona kivuli hiki?"

"Gani?"

Elio alianza kuhisi uwoga.

"Hii hapa. Huioni? Kivuli hiki haihusiani na chochote "alisema, akionesha picha hiyo kwa kidole chake.

"Hii? Ni kivuli cha mti. "

Gaia pia hakuamini, lakini alijaribu kumtuliza kaka yake.

Elio hakutaka dada yake afikirie kuwa alikuwa amerukwa na akili, na akaamua kubadili mada ya majadiliano.

"Lazima tushuke chini. Shangazi Ida amenifanya nije hapa nikuite. Anahitaji msaada wako. "

"Unakaa humu ndani?" aliuliza Gaia akiwa anaruka kuelekea kwa ngazi.

Elio alifikiria kwamba hakukuwa na nafasi kwamba angekaa hapo peke yake.

"Hapana, naenda na wewe" alijibu.



Gaia alimkuta shangazi yake akiwa na kazi ya kuandaa chakula cha jioni na akaanza kumsaidia.

Elio alikuwa karibu kulala katika sofa aliposikia sauti ya Ida.

Je, unafanya nini? Njoo utusaidie. Sio wakati wa kupumzika. Andaa meza, tafadhali.

"Libero yuko wapi?" aliuliza Gaia.

"Hakika anafunga zizi." alijibu Ida. "Elio, ikiwa umemaliza, unaweza kwenda kumwita hapa?"

"Nitaenda." alijitolea Gaia akitabasamu.

"Hapana, nakuhitaji hapa. Mwache ndugu yako aende."

"Ndio." kwa uchovu alijibu Elio, ambaye alikuwa na njaa isiyo ya kawaida.

Alitoka nje ya mlango wa mbele na kumtafuta binamu yake, ambaye alikuwa amekaa kwenye trekta uwanjani, akiangalia angani.

Elio alimwendea na alikuwa na hisia kwamba kila mtu katika familia hiyo alikuwa amekuwa kiziwi: alimwita mara kadhaa, lakini Libero hakujibu.

"Natumai kweli inaambukiza. Angalau nitaweza kujilaza na sitahitaji kusikiliza maagizo ya mtu yeyote. "Alitafakari Elio.

Yeye ilibidi atembee chini ya trekta ili apate jibu.

"Kwanini unapiga kelele?" aliuliza Libero.

"Unapaswa kuingia ndani. Chakula cha jioni tayari "alijibu Elio.

"Njoo juu." Alisema Libero, kana kwamba hakusikia maneno yoyote aliyokuwa akisema Elio.

"Huko juu?"

"Ndio, juu hapa. Nitakuonyesha kitu. "

Elio akapanda juu ya trekta na kuketi karibu naye.

"Angalia jinsi ilivyo nzuri." Alishangaa Libero, akiashiria angani. "Miaka michache iliyopita sikuweza kuiona."

"Nini?" aliuliza Elio huku akijaribu kugundua kile alikuwa akimaanisha.

"Anga." akarudia.

"Anga?"

"Ndio, anga. Ni jambo zuri. Lakini mara nyingi katika maisha yetu hatuinui vichwa vyetu. Wala simaanishi kuangalia hali ya hewa tu, lakini kuifikiria, kwa kimya, kwa njia ile ile tunayofikiria bahari. Ni vile tu ni rahisi kupenda bahari; ndiyo sababu inathaminiwa mara nyingi. Je! Umewahi kusimama na kupendezwa na anga? "

"Hapana."

Unapaswa: Inakuinua na kukufanya uangalie mambo kwa mtazamo sahihi. "

Elio, akishangazwa na akili ya binamu yake, alikaa kimya pamoja naye na akatazama angani kwa muda.

Kutoka weupe wa theluji hadi kijivu cha moshi, mawingu yalikuwa yakielea kati ya vipande viwili vya anga. Ukanda uliokuwa chini yao ulikuwa na kijivu cha risasi, ukanda uliokuwa juu yao ulikuwa wa samawati, uliangazwa na miale ya mwisho ya jua iliyokuwa ikitua. Ukingo wa mawingu ulionekana dhahabu, kana kwamba uliangazwa na nuru ya ulimwengu mwingine, kana kwamba yalikuwepo kuangazia maisha ya zamani. Nyeupe zilikuwa nene kama vilele vikali, zile za kijivu zilikunjana kama mchoro wa mtoto.

Kati yao, moja inaweza kutofautishwa kwa urahisi. Ilikuwa na umbo la nyati na ilikuwa imesimama dhidi ya usuli nyeupe kana kwamba mnyama wa kijivu alikuwa akikimbia kwenye milima nyeupe ya mbinguni. Kama fresco iliyochorwa na Tiepolo


, paa la asili lisilo na mwisho lilikuwa limenyooshwa juu ya kile kinachoonekana, juu ya siri ya uwepo wa roho zetu: ndogo sana, lakini ya milele.

Ghafla, Libero akaruka chini.

"Nimekufa na njaa sasa" alisema, akicheka sana.

"Na wewe, Elio?"

"Ndio."

"Haya, twende tukala. Labda wakati mwingine nitakuendesha tuzunguke na trekta. "

Alisema, akielekea nyumbani kwake.

Elio hakupoteza muda akaanza kumfuata. Alikuwa na njaa pia.






Sura ya nne



Sauti ilikuwa ikinong'oneza masikioni mwake maneno kwa lugha isiyojulikana.



Elio aliamka mapema. Haikuwezekana kutomwitikia shangazi Ida, ambaye alikuwa akiita jina lake kwa sauti ya juu. Nje, ilikuwa inakaribia alfajiri. Aliangalia angani ikipata rangi ya waridi na kwa sekunde moja, alitafakari picha ya machweo ya usiku uliopita na kupata tena hisia hiyo ya amani. Lakini haikudumu kwa muda mrefu kwani alianza kusikia mlio mkali masikioni mwake ambao ulikuwa ukikata roho yake na kumfanya arudie hali yake halisi.

Elio alijikokota hadi jikoni akiwa bado amevaa nguo zake za kulala na akitarajia kiamsha kinywa kitamwamsha.

Shangazi yake, binamu yake na dada yake walikuwa tayari wamevaa na nywele zao zimechanwa vizuri kana kwamba ni saa mbili asubuhi badala ya saa kumi na moja unusu. Kulikuwa na mazingira ya sherehe ndani ya nyumba; Ercole alikuwa akirudi nyumbani kutoka kambi ya majira ya joto na Ida alifurahi kwa kufikiria kuwa na mwanawe nyumbani. Hajakuwa nyumbani kwa siku tano na alikuwa na wasiwasi sana. Alikuwa na wasiwasi kila wakati watoto wao wanapoondoka nyumbani baada ya kile kilichomfanyikia kwa Libero wakati alikuwa mdogo. Hawezi kamwe kutaka kuondoa macho yake kutoka kwao.



Mara tu alipomwona Elio akiwa mkaidi, Sajenti Ida alimtuma aende ili kumfanya afurahi.

Ida alikuwa mwanamke hodari ambaye alikuwa ameimarishwa na ugumu wa maisha. Kufuatia kifo cha mumewe na maswala yaliyomkumba mwanawe, ilibidi ajizoee maisha tofauti kabisa na yale aliyokuwa akiishi mjini na mumewe.

Mgumu na aliyeamua kama alivyokuwa, alishughulikia changamoto hiyo mpya. Wakati mwingine alijiruhusu kulia kwa siri, lakini licha ya hayo hangepoteza nguvu zake.

Sauti yake ya mamlaka ilikuwa ngao yake. Walakini, kwa ndani alikuwa mtamu na laini kama keki.



Baada ya muda, Elio alirudi akiwa amevaa vizuri na kuwa na furaha licha ya mhemko wake mbaya na njaa yake.

Aliweza kunusa harufu ya maziwa na chokoleti, na biskuti mpya ambazo shangazi Ida alikuwa ametengeneza siku moja kabla siku hiyo.

Kulikuwa na maziwa, briocheti zenye umbo la suka katika ladha tofauti: mdalasini, anise, na sesame, anayependa zaidi.

Dada yake na Libero walikuwa tayari wakizitia kwenye maziwa.

Libero akamuuliza:

"Je! Unajua ni nani anayekuja leo?"

Elio alishtuka na swali lake.

"Nani?" alijibu.

"Ercole, kaka yangu mdogo!"

Elio hakusema chochote, lakini alikuwa amesahau kabisa kumhusu Ercole ambaye ni rika lake.

"Kutoka wapi?" aliuliza kana kwamba walikuwa hawajazungumza kuihusu.

"Nini?" akajibu Gaia. "Shangazi Ida alituambia jana."

"Anarudi kutoka kambi ya majira ya joto." alisema Libero akitabasamu.

"Dari inasubiri nyinyi wawili." alidokeza shangazi yao kwa sauti ambayo haikuanzisha majadiliano yoyote. "Haya, Elio, maliza kiamsha kinywa chako na uanze kazi." "Gaia atakuja kukusaidia kidogo. Namuhitaji nimtume apeleke ujumbe. "

"Elio alikunywa maziwa yake kidogo kidogo, akifarijika kwa wazo la kukaa pekee yake kwenye dari. Alifurahi kwamba angeweza kurudi kusikiliza muziki wake kwenye kichezaji chake cha mp3.

Alitafuta nyumba nzima lakini hakuipata mahali popote. Alirudi jikoni na kuuliza:

"Kuna mtu ameona kicheza mp3 changu?"

"Kwa bahati mbaya, kuna kitu kilichofanyikia hapo jana. Ulikuwa umeiacha kwenye sofa. Nilipofungua kitanda cha sofa, kilikwama kati ya mfumo wa fremu...Hakuna mengi yamebaki, lakini nimefanikiwa kuokoa kadi ya kuhifadhi data." alisema shangazi yake, ambaye alichukua kadi hiyo ya kuhifadhi data kutoka kwa sahani na kumpa.

"Siku imeanza kwa njia mbaya" aliendelea kufikiria Elio. Alipanda ngazi ambazo zinaelekea kwenye dari kwa kasi yake ya kawaida na kuwasha taa.

Mambo yalikuwa yamerundikana kila mahali. Alilazimika kusafisha kila kitu na kutafuta mahali pa kuweka vitanda viwili. Mawazo tu kuihusu yalikuwa mengi sana kwake. Kwa hivyo, aliamua kufungua dirisha kubwa la kati ili kuingiza hewa safi na mwanga wa mchana, na alikusudia kukaa chini na kumsubiri Gaia.

Lakini basi, kitu kilimshika macho. Kilikuwa kitabu kilichowekwa kwenye sanduku la zamani la mbao ambacho kilionekana kuwa cha kushangaza sawa na kitabu ambacho yule mzee alikuwa akisoma kwenye gari moshi.

Ilikuwa ulinganifu usio wa kawaida. Hakika haikuwa kitabu cha kawaida sana, ambacho kilimfanya awe na wasiwasi. Ghafla, taa ilizima na Elio akaanza kusikia sauti ile isiyo ya kawaida kwamba, kama ishara mbaya, alikuwa akinong'oneza masikioni mwake maneno katika lugha isiyojulikana.

Ingawa alijua haiwezekani, Elio aliogopa kwamba mzee huyo angeweza kusimama pale pale pamoja naye, gizani. Alitafuta swichi ya taa, lakini hakuweza kuiwasha. Balbu ya taa lazima ilipasuka. Hofu kubwa ilimchukua. Sauti ilizidi kuongezeka na kuongezeka na ikaendelea kujirudia kichwani mwake. Alikuwa akingangana gizani ili kufika dirishani, akikokota vitu vyote ambavyo alikuwa akikutana navyo.

Alipofika kwenye mpini, akagundua kuwa dirisha lilikuwa limefungwa na kuanza kupiga ngumi kwenye glasi akitarajia itafunguka.

Alikuwa akitetemeka na alikuwa anatiririkwa na jasho baridi.

Ghafla, taa ikawaka. Elio aligeuka, alitaka kupiga kelele, lakini koo lake likasonga.

Kisha akamwona Gaia.

"Elio, uko sawa? Kuna nini na kelele hizi zote? Umeumia?"

Mvulana huyo, ambaye alikuwa mweupe kama shuka na alikuwa akitetemeka, alionekana kufadhaika.

Gaia alimkumbatia kwa nguvu na kwa wasiwasi alimnong'oneza:

"Je! Kila kitu ni sawa? Ilitokea tena, sivyo? Hicho kitu kinachokufadhaisha... "

Elio hakujibu wala kumkumbatia. Alikuwa bado mbali, mbali sana, ndani ya mawazo yake. Hakuweza kuhisi kwenye ngozi yake joto la kukumbatiwa. Ilikuwa ni kana kwamba alikuwa ameumbwa kwa mawe.

Gaia alimwachilia kidogo na kisha Elio akapata fahamu.

Jambo la kwanza alilofanya ni kuangalia ikiwa hati hiyo isiyo ya kawaida ilikuwa bado mahali ambapo alikuwa ameiona, au ikiwa alikuwa ameifikiria tu.

Kwa bahati mbaya, ilikuwa bado iko. Na sura yake ikawa baridi kwa mara nyingine.

Gaia aligundua kile kilichokuwa kimetokea na akatembea kuelekea mahali kitabu hicho cha zamani ilikuwa. Alitaka kuona ikiwa ni sababu ya shida ya kaka yake. Alichambua mwelekeo wa mahali Elio alikuwa akitazama.

Alikuwa akiangalia kabisa kitabu kile cha zamani. Aligeuka na kuishika. Na akiwa na kitabu mikononi mwake, alimwambia:

"Je! Hii ndio sababu umekuwa na hofu sana?"

Elio hakusema hata neno moja.

"Elio, ongea nami. Siwezi kukusaidia ikiwa unasisitiza kutoongea nami "

"Ile gari moshi." akanong'ona Elio.

"Ile gari moshi? Unamaanisha nini?"

"Niliona kitabu sawa na hicho kwenye ile gari moshi."

"Ni nini cha kushangaza kuhusu hayo?"

"Huyu mzee wa ajabu alikuwa akikisoma wakati ulikuwa umeeenda kwa gari la mgahawa. Alikuwa amekaa kwenye safu karibu na yangu.

"Watu wengi husoma vitabu wanapokuwa safarini."

"Lakini sio kitabu cha kawaida, je! Huwezi kukiona?" alijibu Elio, ambaye alikuwa amekasirika.

Kwa kweli, Gaia hakuwa ameona jinsi jalada la kitabu hicho lilikuwa la kipekee, na alionekana kushangaa zaidi wakati alifungua.

Iliandikwa kwa lugha ya kigeni. Picha zarangi nyeusi na nyeupe zilionesha picha isiyo ya kawaida iliyosimama kwenye misitu na mwezi kamili. Nyingi za takwimu hizo zilikuwa za kusumbua,

lakini alijifanya kutoziona. Alifunga kitabu mara moja na kukitupa pembeni.

"Haya, ni ulinganifu tu. Ni kitabu cha zamani tu. "

Elio alikaa kimya; masikio yake yalikuwa yakisikia mlio tena.

Msichana mchanga alijaribu kumvuruga, ingawa picha hizo za kupendeza hazikuacha akili yake.

"Haya, nisaidie kusogeza hizi sanduku kuelekea pale kuna taa. Na hebu tutengeneze nafasi chini ya mahali anga inaonekana. Hapo ndipo ninapotaka kitanda chetu kiwe. Kwa bahati mbaya, tutalala kitanda kimoja, na ninataka kulala chini ya mwangaza wa nyota. "

Walifanya kazi asubuhi yote kwa mwendo mzuri. Gaia alifanikiwa kumvuruga Elio na maongezi yake na alionekana akijibu kwa nguvu zaidi baada ya kile kilichotokea.

Walifanya kazi ya kusafisha kila kitu alasiri yote hadi shangazi Ida alipowahimiza wajipumzishe kidogo. Usiku huo Ercole alikuwa akirudi nyumbani na walitaka kusherehekea.

Libero alikuwa ameahidi kwamba atawapeleka kwenye densi kwenye sherehe ya mavuno ambayo ingefanyika mjini.

Walisikia mlio wa honi ya gari ikipigwa. Ilikuwa basi la zamani la eneo hilo ambalo hupita mara mbili kwa wiki. Baada ya kupitia vitongoji tofauti vya jiji, mwishowe ingefika mji wao. Kawaida, watoto wangeitumia kurudi kutoka kambi ya majira ya joto huko Tresentieri, eneo lisilo mbali sana na mji mkuu.

Libero akatoka nje ya nyumba, na, kama kawaida, akamwinua kaka yake, ambaye hakuweza hata kubeba mkoba wake mkubwa, na akamzungusha hadi mlango wa mbele. Baada ya Ercole kufanikiwa kutoka kwenye nafasi ya "kubana", ilibidi ashughulike na mama yake.

Alifurahi kuhusu dhihirisho hilo la mapenzi, lakini ilionekana kwake walikuwa wametia chumvi ikizingatiwa kwamba alikuwa nje kwa siku tano tu.

Alimbusu Gaia kwa upendo kwenye mashavu yake, ambaye aliona ni mrembo sana, na kwa upole akasema hujambo kwa Elio, ambaye Runinga na michezo yake ya video anayoipenda haikuwepo.

Ercole alikuwa na umri sawa na Gaia, na kama shujaa wa Ugiriki, alikuwa mrefu, pande la mtu na alikuwa katika timu ya mieleka ya mtaani.

Nywele zake nyeusi zilichanwa kwa mtindo wa vijana. Macho yake meusi na ngozi yake ya mzeituni ilimfanya aonekane mkali zaidi kuliko jinsi anavyokuwa kwa kawaida. Kwa kweli, alikuwa kijana mwenye tabia nzuri, asiye na uwezo wa kushikilia kinyongo.



Chakula cha jioni kilitolewa mapema kuliko kawaida ili wawe na muda wa kutosha wa kujiandaa kwa sherehe. Walikuwa na muda kabla ya sherehe yenyewe, lakini Ida alikuwa ameandaa karamu halisi ya hafla hiyo, na walihitaji wakati wote huo kupitisha kwa kila mtu sahani zote.

Baada ya hapo, walikuwa tayari kuanza.



Wanaume wote ndani ya nyumba walilazimika kungojea muda mrefu zaidi ya ilivyotarajiwa, bila shaka. Ida na Gaia walikuwa wakichukua muda mwingi. Elio hakuwa katika mhemko. Zaidi ya hayo alidhani kwamba mavazi ambayo alikuwa amevaa siku nzima yalikuwa yafaayo zaidi. Ercole alivaa suruali ya jinzi na kupaka nywele zake mafuta mengi.

Kati ya wavulana, Libero alichukua muda mrefu. Hakutoka nje ya chumba chake cha kulala hadi alipokuwa tayari kabisa. Alionekana kupendeza na suruali yake ya Capri ya rangi ya samawati na shati lake lenye rangi mseto ambalo lingeonekana lisilo nzuri kwa mtu yeyote, lakini lilikuwa nzuri kwake.

Macho yake yalikuwa yaking'aa. Ilikuwa moja ya sherehe alizofurahia zaidi.

Mara tu kila mtu alipokuwa tayari, Elio alijaribu kutoroka mateso hayo, lakini alishikwa na shauku ya shangazi yake, ambaye alionekana kutotambulika. Alikuwa amevaa nguo nyeusi yenye maua, viatu vyenye visigino virefu na nywele zake zilikuwa huru begani. Zaidi ya hayo, alikuwa amejipaka vipondozi kwenye uso wake. Alimchukua kwa kumshika mkono wake na kumsindikiza nje.



Njiani, walipendezwa na taa, vibendera na mapambo ambayo yaliwekwa na watayarishaji wa tamasha la mwaka huo.

Pembeni ya barabara, marobota ya nyasi katika maumbo yote yalikuwa yamepamba mji.

Katikati mwa jiji, eneo la kumbukumbu ya vita ilizungukwa na magurudumu makubwa yaliyotengenezwa kwa majani kavu.

Eneo la mraba kuu lilikuwa mwenyeji wa jukwaa ambalo bendi itaandaa gwaride.

Pande zote za uwanja wa densi, viti vyote vilikuwa vimekaliwa na wazee, ambao walikuwa wakipiga soga na kusubiri kushangilia densi zote za vijana. Watoto wadogo walikuwa tayari wakizunguka kwenye uwanja wa densi, wakiiga watu wazima ambao italazimika kuwaepuka wakati wa densi.

Usiku huo kila mtu mjini alikuwa akiongea kuhusu kuwasili kwa Gaia na Elio. Wazee na watu wazima walikuwa wakikumbuka nyakati za zamani wakati ndugu wawili wangekuja mjini.

Watu walikuwa na maoni tofauti: Baadhi yao wangewakumbuka kama watoto jeuri na ambao wanaweza kukasirika kwa uraisi, wengine wao wangewakumbuka kama watoto wazuri. Rafiki wao wa zamani, kwa upande mwingine, walikuwa wakikumbuka zamani nyakati ambazo wangekwepa shule na kupotea mashambani.

Mtu anaweza kusema kwamba Elio alionekana kama baba yake, wengine wangesema kwamba Gaia ndiye anayeonekana kama babaye. Wengine wangejaribu kutatua siri hiyo kwa kusema kwamba wanafanana na babu zao.

Wakati huo huo, bendi ilikuwa ikifanya mazoezi ya gwaride. Kila kitu kilikuwa kinakaribia kuwa tayari. Mwenyeji, au kwa usahihi zaidi, yule mtu kwamba kila mwaka alikuwa na jukumu la kuongea kwenye jukwaa, alialikwa jukwaani na mwakilishi wa serikali za mitaa.

Alimaliza hotuba yake kwa kuwashukuru wafadhili, wakati wakazi wote wa mji walionekana kutovutiwa kabisa na kile alichokuwa akisema na kuanza kupiga miayo. Muda mfupi baada ya hapo, watazamaji walipiga makofi wakitumaini kwamba mwenyeji huyo alikuwa amemaliza hotuba yake kabisa na hatimaye ataiachia bendi hiyo nafasi.

Ilipotangazwa kuwa mwenyeji anaondoka jukwaani, makofi makali yalishuhudiwa. Kondakta wa orchestra alipanda jukwaani na kuanza akipunga kijiti kwa washiriki. Kwa wakati uo huo, wapiga tromboni waliingia, ikifuatiwa na ngoma, kisha na saksafoni na mwishowe wapiga zumari.

Libero alikuwa wa kwanza kujibwaga kwenye uwanja wa densi, akifuatana na mpenzi wake ambaye angeanza naye densi kila wakati. Kwa kushangaza, Libero alikuwa mcheza densi mzuri na wanawake wote wa huko walifurahia kucheza densi naye. Angekuwa makini kwa wasichana wadogo na wanawake wakubwa. Alipenda kucheza densi na aliweza kuwasilisha shauku yake isiyopendeza kwa wenzi wake.

Sakafu ya densi ilijaa watu wakicheza densi. Gaia alikuwa akipokea mialiko mingi ya kucheza deni na hakuwa akirudi nyuma.

Kwa sekunde, Elio alihisi hisia isiyo ya kawaida. Bila hata kujua, miguu yake ilikuwa imeanza kucheza densi.

Mara tu ngoma ilipozidi kujitokeza, shangazi yake alimshika kwa mkono wake ulioning'inia na kumfanya acheze na kujizungusha.

Ajabu hakupinga uamuzi huo. Kwa papo hapo, alihisi densi ikiingia mwilini mwake. Alikuwa akiburudika sana hivi kwamba mashavu yake yakaanza kuuma kwa sababu ya upotozi usio wa kawaida wa misuli ya usoni ambayo hakuwa ameipata kwa miaka.

Aliacha kucheza densi mikononi mwa shangazi yake na kujiunga na wasichana wengine kadhaa ambao walivutia na walikuwa wakimwangalia wakicheka.

Baada ya kumaliza kucheza na msichana wa mwisho, Elio alirudi kwenye kiti chake. Aliweza kuhisi damu yake ikitiririka kupitia viungo vyake. Ghafla, alianza kusikia ile mlio usio wa kawaida ikilia kwenye maskio yake, ambayo ilimlazimisha aondoke kwenye uwanja kuu. Muziki ule ule ambao alikuwa akicheza hadi dakika chache zilizopita ulianza kuumiza maskio.

Alitembea kuelekea kwenye nyasi kando ya kanisa, ambapo matrekta ya zamani yalioneshwa. Kikundi cha watoto kiliendelea kuyaangalia na kukimbia wakizunguka.

Elio alikaa kwenye kona yenye giza na kuanza kuwaangalia.

Vicheko hivyo vyote vilikuwa vikisikika katika akili yake na vikilikuwa vikimkumbusha furaha ya zamani iliyosahaulika kwa muda mrefu.

Alikuwa na wivu kwa mtoto ambaye alikuwa akimkimbilia baba yake kwa furaha na kumshika mkono. Alipoona hivyo, kumbukumbu ya zamani ilirudi akilini mwake: akakumbuka joto na manukato ya mkono wa baba yake.

Alianza kuhisi maumivu makali mwilini mwake. Hakuweza kufikiria. Alishika kichwa chake kwa mikononi yake. Alikuwa baridi.

"Elio, unafanya nini hapa peke yako? Una maumivu? "

Shangazi Ida, ambaye alimfuatilia usiku mzima, aliketi karibu naye. Elio hakujibu.

Ida aliweka mkono wake kwenye mabega yake na kwa upole akamshika kifuani katikati ya mikono yake. Lakini Elio hakuweza kusikia joto la kukumbatiwa. Kulikuwa na baridi katika ulimwengu wake.



Wakati wa kurudi shambani, Gaia hakuweza kuacha kuzungumza kuhusu usiku wake wa kufurahisha na rafiki zake wapya.

Kwa mara ya kwanza walilala kwenye dari. Walikuwa wameweka kitanda chini ya mwangaza wa angani ili Gaia alale akiangalia nyota, na yeye pia.





Конец ознакомительного фрагмента. Получить полную версию книги.


Текст предоставлен ООО «ЛитРес».

Прочитайте эту книгу целиком, купив полную легальную версию (https://www.litres.ru/pages/biblio_book/?art=64891831) на ЛитРес.

Безопасно оплатить книгу можно банковской картой Visa, MasterCard, Maestro, со счета мобильного телефона, с платежного терминала, в салоне МТС или Связной, через PayPal, WebMoney, Яндекс.Деньги, QIWI Кошелек, бонусными картами или другим удобным Вам способом.



ROBO MWEZI: Dunia ambayo Elio anatorokea huenda isiwe kipande cha mawazo yake, lakini utando uliofumwa kwake. Wakati wa likizo kijijini atapata fursa ya kukutana na mlinzi atakayemfichulia ukweli. Kando na kundi la kuchekesha, wa ukweli na wa kimawazo, atapambana ili kujipatia tena uhuru wake. Vituko vya mtoto huyo vitakufanya ufahamiane na mapepo, mlinzi, kifuli, vidonda, tulivu za miujiza, na utasafiri kote duniani ukitumia taa za trafiki,ukizunguka mbuyu au kupaa ndani ya mpira wa barafu

Как скачать книгу - "Robo Mwezi" в fb2, ePub, txt и других форматах?

  1. Нажмите на кнопку "полная версия" справа от обложки книги на версии сайта для ПК или под обложкой на мобюильной версии сайта
    Полная версия книги
  2. Купите книгу на литресе по кнопке со скриншота
    Пример кнопки для покупки книги
    Если книга "Robo Mwezi" доступна в бесплатно то будет вот такая кнопка
    Пример кнопки, если книга бесплатная
  3. Выполните вход в личный кабинет на сайте ЛитРес с вашим логином и паролем.
  4. В правом верхнем углу сайта нажмите «Мои книги» и перейдите в подраздел «Мои».
  5. Нажмите на обложку книги -"Robo Mwezi", чтобы скачать книгу для телефона или на ПК.
    Аудиокнига - «Robo Mwezi»
  6. В разделе «Скачать в виде файла» нажмите на нужный вам формат файла:

    Для чтения на телефоне подойдут следующие форматы (при клике на формат вы можете сразу скачать бесплатно фрагмент книги "Robo Mwezi" для ознакомления):

    • FB2 - Для телефонов, планшетов на Android, электронных книг (кроме Kindle) и других программ
    • EPUB - подходит для устройств на ios (iPhone, iPad, Mac) и большинства приложений для чтения

    Для чтения на компьютере подходят форматы:

    • TXT - можно открыть на любом компьютере в текстовом редакторе
    • RTF - также можно открыть на любом ПК
    • A4 PDF - открывается в программе Adobe Reader

    Другие форматы:

    • MOBI - подходит для электронных книг Kindle и Android-приложений
    • IOS.EPUB - идеально подойдет для iPhone и iPad
    • A6 PDF - оптимизирован и подойдет для смартфонов
    • FB3 - более развитый формат FB2

  7. Сохраните файл на свой компьютер или телефоне.

Видео по теме - Kwanini Mwezi huonekana nusu robo mzima robotatu au haupo kabisa fahamu kwa kina kuandama kwa mwezi

Книги автора

Рекомендуем

Последние отзывы
Оставьте отзыв к любой книге и его увидят десятки тысяч людей!
  • константин александрович обрезанов:
    3★
    21.08.2023
  • константин александрович обрезанов:
    3.1★
    11.08.2023
  • Добавить комментарий

    Ваш e-mail не будет опубликован. Обязательные поля помечены *